Bonyeza link hii kuangalia : https://matokeo.necta.go.tz/results/2024/pslexj6/psle.htm |
Tuesday, October 29, 2024
Sunday, August 18, 2024
Sarufi za Kiswahili
SARUFI
Sarufi nimfumo na kanuni za lugha
zinazomwezesha mtumiaji wa lugha kuitumia lugha
husika kwa usahihi. Mfumo huo humwezesha
mzungumzaji kutunga sentensi zisizo na kikomo
ambazo hukubalika na wazawa wa lugha
wanaoifahamu lugha hiyo barabara. Hivyo ni dhahiri
kwamba kila lugha ya mwanadamu huwa na
mpangilio na sheria zinazoilinda ili kuifanya kuwa
toshelevu na sanifu, na uzingatiwaji wa kanuni na
taratibu hizo kwa mtumiaji humfanya na
kumtambulisha kama mmilisi wa lugha hiyo.
Sheria za lugha zimegawanyika katika
makundi manne yanayojulikana kama matawi ya
Sarufi ambayo ni pamoja na; matamshi, maumbo,
muundo na maana.
1. SARUFI MATAMSHI
Sarufi matamshi ni tawi la sarufi ambalo
limejikita katika kuchunguza sauti na
matamshiyanayotumika katika lugha Fulani na
kulinda matumizi sahihi ya matamshi hayo baina ya
watumiaji wa lugha hiyo. Lugha ya Kiswahili kama
zilivyokuwa lugha zote duniani ina matamshi ya aina
mbili; Irabu na konsonanti.
A. Irabu
Irabu ni aina ya vitamkwa ambavyo
hutolewa pasi na kuwepo kizuizichochote katika
mkondo hewa utokao mapafuni ukipitia katika
chemba ya kinywana chemba ya pua kwenda nje.
Lugha ya Kiswahili inazo Irabu tano ambazo ni; /
a/, /e/, /i/, /o/, na /u/.
B. Konsonanti
Konsonanti ni aina ya sauti ambazo
hutamkwa kwa kuzuia mkondo hewa kutoka
mapafuni, ukipitia chemba ya kinywa na chemba ya
pua kwenda nje. Katika lugha ya Kiswahili zipo
jumla ya konsonanti zifuatazo; /b/, /ch/, /d/, /dh/, /
f/, /g/, /gh/, /h/, /j/, /k/, /l/, /m/, /n/, /ny/, /ng'/, /
p/, /r/, /s/, /sh/, /t/, /th/, /v/, /w/, /y/ na /z/.
2. SARUFI MAUMBO
Hili ni tawi la sarufi ambalo hujishughulisha
na uchunguzi wa maumbo mbalimbali ya maneno
katika lugha ya Kiswahili. Maumbo hayo ni; silabi,
mofimu na neno lenyewe.
A. Silabi
Silabi ni kipashio cha kifonolojia
kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za
Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama
fungu moja la sauti. Kuna aina mbili za silabi, yaani
silabi fungenasilabi huru. Silabi huru ni zile ambazo
huishia na irabu.
Kwa mfano; la, ma, kwa, mba, n.k.
Ilhali silabi funge ni zile zinazoishia na
konsonanti ambapo katika lugha ya Kiswahili ni
nadra kuzipata maana lugha hii inatumia silabi huru
lakini hupatikana katika maneno ya Kiswahili
yanayokopwa kutoka katika lugha nyingine.
Kwa mfano: alhamisi – a-l-ha-mi-si; taksi
- ta-k-si
Miundo ya Silabi za Kiswahili
a. Muundo wa irabu peke yake (I) - Yapo maneno
katika lugha ya Kiswahili yanayoundwa na irabu
peke yake kama silabi. Mfano; u+a = Ua, o+a = Oa,
a+u = Au, n.k.
b. Muundo wakonsonanti pekee (K) – Kiswahili hakina
maneno mengi yanayoundwa na silabi pekee
isipokuwa maneno machache ambayo huwa ni ya
nazali /M/ na /N/ na huwa zinatumika ama
mwanzoni au katikati ya neno. Mfano; m+ke = Mke,
m+bwa = Mbwa, n+chi = N chi n.k.
c. Muundo wa konsonanti na irabu (KI) – Katika
muundo huu konsonanti hutangulia irabu. Mfano; b
+a = Ba, k+a = Ka n.k.
d. Muundo wa konsonanti mbili na irabu (KKI) – Katika
muundo huukonsonanti mbili hutangulia irabu. Mara
nyingi konsonanti ya pili huwa ni kiyeyusho. Mfano;
k+w+a = Kwa, m+w+a = Mwa, b+w+a = bwa, n+d
+e = Nde, n.k.
e. Muundo wa konsonanti tatu na irabu (KKKI) –
Muundo wa namna hii hujitokeza katika maneno
machache. Mfano; Ba mbwa, Tingw a, Tindwa,
Mbw a, n.k.
f. Muundo wa silabi funge – Huu hujitokeza katika
maneno machache ambayo huwa ya mkopo. Mfano;
Il-ha-li = Il hali, Lab-da = Lab da
B. Mofimu
Mofimu ni kipashio kidogo kabisa cha
lugha ambacho kina uwezo wa kusitiri maana ya
neno ambalo kwalo limeundwa. AU ni kipashio
kidogo kabisa cha lugha chenye maana kisarufi.
AINA ZA MOFIMU
Mofimu huru ni aina ya mofimu ambayo
huweza kusimama pekee na kujitosheleza kimaana
yaani huwa na sifa ya neno. Mfano; mama, Baba,
Dada, Kaka, Mjomba, Shangazi n.k. Kwa kuangalia
utagundua kuwa mofimu huru haziwezi
kugawanyika zaidi na kubeba maana kisarufi, kwa
maana kwamba mofimu 'baba' ikigawanywa ba-ba,
'ba' hii haina maana yoyote kisarufi zaidi ya kuwa
silabi.
Mofimu tegemezi ni aina ya mofimu
ambayo huweza kuvunjwavunjwa na kubeba maana
kisarufi, mofimu tegemezi hutegemeana ili kuleta
maana kamili ya neno.
Mfano; neno 'anakula' limeundwa na
mofimu zifuatazo:- [a-na-kul-a] ambazo kila moja
hubeba dhana Fulani ya kisarufi.
VIAMBISHI
Ni mofimu zinazopachikwa nyuma au
mbele ya mzizi wa neno ili kubadilisha dhana ya
neno. Kwa kuwa mofimu hizo hupachikwa sehemu
mbili tofauti, tunapata aina mbili za viambishi kwa
mujibu wa nafasi zake katika nenoyaani; viambishi
awaliambavyo hupachikwa mwanzoni au nyuma ya
mzizi wa neno,viambishi katiambavyo hupachikwa
katikati ya neno (Kiswahili hakina viambishi hivi) na
viambishi tamatiambavyo hivi hupachikwa mbele au
mwishoni mwa mzizi wa neno. Mfano:
VIAMBISHI
AWALI
MZIZI WA
NENO
VIAMBISHI
TAMATI NENO JIPYA
A na chez ew a Anachezewa
Wa li chez ean a Walichezeana
Tu ta chez e a Tutachezea
1. Viambishi awali Hivi hupachikwa kabla ya mzizi wa
neno na huwa ni vya aina tisa:
i. Viambisha awali vya nafsi- hivi hudokeza
upatanishi wa nafsi katika kitenzi, zipo nafsi tatu,
nafsi ya kwanza, ya pili, nay a tatu.
NAFSI UMOJA UWINGI
Ya Kwanza Ni- Tu-
Ya Pili U- M-
Ya Tatu A- Wa-
Mfano: Ni nalima, Tu nacheza
ii. Viambishi awali vya ngeli — hivi hupatikana
mwanzoni mwa nomino au vivumishi ili kudokeza
hali ya umoja na uwingi.
Mfano: Mtu (umoja) — Watu (uwingi); Msafi (umoja)
– Wasafi (uwingi)
iii. Viambishi awali vya ukanushi - hivi hudokeza hali
ya uhasi wa tendo. Huwakilishwa na mofimu (ha-)
na (si-)
Mfano: Amekula (uyakinifu) – Hajala (ukanushi),
Nakula (uyakinifu) – Sili (ukanushi)
iv. Viambishi awali vya Njeo - hivi hudokeza nyakati
mbalimbali ambazo ni wakati uliopita, uliopo na ujao.
NYAKATI MOFIMU
Uliopo -na-
Uliopita -li-
Ujao -ta-
Mfano: Mli tuona, Uta kuja
v. Viambishi awali vya hali — hivi hudokeza hali mbili
za nyakati ambazo ni mazoea ambayo
huwakilishwa na mofimu {hu} na timilifu
inayowakilishwa na mofimu {me}.
Mfano: Hu cheza, Ame lima
vi. Viambishi awali vya masharti — hivi hudokeza hali
ya masharti au uwezekano katika tendo. Mofimu
hizo ni kama –ki-, nge-, ngali- n.k.
Mfano: Uki ja, Unge kuja, Angali mkuta
vii. Kiambishi cha urejeshi wa mtenda (kiima) — mhiki
hudokeza urejeshi wa nomino inayotenda katika
kitenzi.
Mfano: Aliye kuja {-ye-} hudokeza urejeshi wa
mtenda.
viii. Kiambishi kiwakilishi cha mtendwa au mtendewa
(shamirisho) — hivi huwakilisha mtendwa au
mtendewa wa jambo.
Mfano; Nili mpiga, Uli ukata, Nime ipenda,
Wame ni teta.
ix. Kiambishi awali cha kujirejea (kujitendea) — hiki
huwakilishwa na mofimu (-ji-)
Mfano: ku jipenda
2. Viambishi tamati — Hivi hudokeza kauli mbalimbali
za vitenzi.
Mfano: Anacheza — Kutenda; Unachezw a —
Kutendw a; Utachezew a — Kutendew a; Nimemlia —
Kutende a; Wamewasomesh a — Kutendesh a n.k.
Mzizi Kiambishi
cha Kauli
Kiambishi
tamati
maana
Neno jipya Kauli Viambishi
vya kauli
Chez a Cheza Kutenda -a
e a Chezea Kutendea -e-
Pig ian a Pigiana Kutendeana -ian-/-
ean-
iw a Pigiwa Kutendewa -iw-/ew-
Som esh a Somesha Kutendesha -ish-/
esh-
eshw a Someshwa Kutendeshwa -ishw-/
eshw-
Lim ik a Limika Kutendeka -ik-/-
ek-
an a Limana Kutendana -an-
w a Limwa Kutendwa -w-
DHANA YA MZIZI NA SHINA LA KITENZI
Mzizi wakitenzi ni sehemu ya neno
inayobakia mara baada ya kuondoa viambishi vyote
vya awali na tamati katika neno hilo. Mfano: - a-na-
chez-a {-chez-}, m-ku-lim-a {-lim-}
Mzizi funge ni ule ambao hauwezi
kujikamilisha kimaana yaani hauwezi kusimama
kama neno. Mfano; -lim-, -chez-, -imb- n.k.
Mzizi huru ni ule ambao huweza
kusimama kama neno na ukichanganuliwa zaidi
hupoteza maana yake ya msingi. Mfano; Kinu, Kazi,
Arifu, Sali n.k.
Shina la kitenzi ni sehemu ya neno
ambayo huongezwa viambishi fuatishi (tamati) au
nisehemu ya neno ambayo hubakia baada ya
kuondolewa viambishi tangulizi. Mfano:- chez+a =
cheza, lim+a = lima. Sehemu hii ya neno hutumika
kuundia neno jipya. Shina sahili – hili ni shina
ambalo huundwa na mofimu moja tu ambayo ni
mzizi wa neno hilo, huwa ni mofimu huru, Mfano;
Kesho, jana, kitabu, jarida n.k.
Shina changamano – shina hili huundwa
na mzizi na kiambishi tamati maana. Mfano; cheka,
lala, lia, kula n.k.
Shina ambatani – shina hili huundwa na
mofimu mbili ambazo ni huru. Mfano; mwana +
kwenda = mwanakwenda , mbwa + mwitu =
mbwamwitu
UAMBISHAJI NA MNYUMBULIKO WA MANENO
Uambishaji
Uambishaji ni ule utaratibu wa kuongeza
viambishi katika mzizi wa neno, ili kulipa neno
maana ya ziada. AU ni hali ya kubadilishabadilisha
mofimu katika mzizi wa neno ili kuonesha
upatanisho wa kisarufi katika tungo hiyo.
Kiambishi
Kiambishi ni sehemu (mofu) ambayo
huambikwa kwenye mzizi wa neno ili kulipa neno
hilo maana ya ziada. Tunapopachika viambishi
hivyo mwanzoni mwa mzizi wa neno hali hiyo
huitwa ‘uambishaji’ . Uambishaji upo wa aina mbili;
Unyambuaji au unyambulishi: Huu ni aina ya
uambishaji unaosababisha neno kubadilika kutoka
kategoria moja hadi nyingine. Na Mnyambuliko: Ni
aina ya uambishaji ambao huhusisha kurefusha
nenona kuliweka katika hali tofauti za katagoria
ileile.
Uambishaji wa kategoria mbalimbali za maneno
Uambishaji wa vitenzi – Uambishaji wa
vitenzi hujitokeza kwa kutegemea dhima tofauti
tofauti za mofimu kama vile:
i. Viambishi vya nafsi
ii. Viambishi vya njeo
iii. Viambishi vya ukanushi
iv. Viambishi vya urejeshi
v. Viambishi vya hali
vi. Na viambishi vya kujitendea
Mfano: mzizi –lim- unaweza kupachikwa
viambishi hivyo na kuweza kubadilika kidhana kama
ifuatavyo:
A-na-lim-a
Hu-lim-a
U-me-lim-a
Ni-na-vyo-lim-a n.k.
Uambishaji wa majina Uambishaji wa
majina huwa unazingatia upatanisho wa kisarufi
kimofolojia ambao hujikita katika kuangalia alomofu
tofauti zinazowakilisha ngeli moja katika umoja na
uwingi wa majina hayo.
Kwa mfano:
UMOJA WINGI ALOMOFU
m-tu wa-tu M/WA
m-ti mi-ti M/MI
ki-ti vi-ti KI/VI
u-gonjwa ma-gonjwa U/MA
Ø-fisadi ma-fisadi Ø/MA
Ø-kaka Ø-kaka Ø/Ø
Uambishaji wa vielezi Vielezi katika lugha
ya Kiswahili havitokani na kategoria nyingine ya
maneno, bali ni maneno ya kawaida yanayopatikana
katika lugha na si rahisi kupachika mofimu yoyote
katika maneno hayo isipokuwa vielezi vichache
ambavyo hupatikana kwa kupachikwa kiambishi
awali cha namna {ki-} katika kivumishi au nomino
mfano: ki-jinga, ki-janja, ki-toto, ki-raia, ki-puuzi
n.k.
UNYAMBULISHAJI
Ni hali ya kupachika viambishi tamati
katika mzizi wa neno. Mofimu hizo huitwa mofimu
fuatishi.
Unyambulishaji wa kategoria mbalimbali za maneno
ya Kiswahili
i. Viwakilishi. Mfano: Mimi = miye, Sisi = siye,
Ambalo, Ambacho, Ambao, Ambaye n.k.
ii. Majina. Mfano: Nyumba+ni = Nyumbani, Shamba+ni
= Shambani, n.k.
iii. Vivumishi. Mfano: Safi = Safisha, Refu = Refusha
n.k.
iv. Vitenzi. Mfano: Lima-limika-limishwa-limwa-
limiana-limiwa n.k.
Ukitazama kwa makini utangundua
kwamba unyambulishaji mara nyingi hubadilisha
neno kutoka katika kategoria moja na kuipeleka
katika kategoria nyingine.
DHIMA ZA UNYAMBULISHAJI
i. Kuongeza msamiati wa lugha ya Kiswahili.
ii. Kuzalisha kauli mbalimbali za vitenzi vya Kiswahili.
iii. Hupanua maana ya neno.
TABIA ZA VITENZI VYA KISWAHILI
Vitenzi vya Kiswahili huwa na tabia tofauti
tofauti zinazotokana na dhima za mofimu ambazo
hupachikwa katika vitenzi hivyo, hivyo kulingana na
dhima za mofimu, vitenzi vya Kiswahili huwa na
tabia zifuatazo:
i. Kutambulisha nafsi. Mfano: A nayesoma
ii. Kutambulisha tendo. Mfano: Cheza, Lima, Imba n.k.
iii. Kutambulisha wakati. Mfano: U likuja
iv. Kutambulisha hali ya uyakinishi na ukanushi. Mfano:
A nacheka – Ha cheki.
v. Kutambulisha kauli mbalimbali za tendo. Mfano:
cheza-chezwa-chezewa-chezeka n.k.
vi. Kutambulisha hali ya tendo. Mfano: Huimba,
A me kula.
vii. Kuonesha urejeshi wa mtenda, mtendwa na
mtendewa ambao hujidhihirisha katika ngeli ya
nomino iliyotajwa kwa kuzingatia upatanisho wa
kisarufi. Urejeshi huo ni wa O-rejeshi. Katika
urejeshi huo vitenzi hubeba viambishi ngeli vya –O-
isipokuwa kama nomino ni ya ngeli ya kwanza
umoja ambapo hutumia –e- badala ya –O-.
Mfano:
NGELI KIAMBISHI CHA O-
REJESHI MFANO
A-WA -YE- na -O- Aliyepiga / Walio kuja
U-I -O- na -YO- Ulio katwa / Ili yo katwa
LI-YA -LO- na -YO- Lililo chanika / Yali yochanika
KI-VI -CHO- na -VYO- Kilicho vunjika / Vili vyo vunjika
I-ZI -YO- na -ZO- Ili yofungwa / Zili zofungwa
U-ZI -O- na -ZO- Ulio katika / Zili zokatika
U-YA -O- na -YO- Ulio nipata / Yali yo nipata
KU -KO- Kuli kotokea
PA-MU-
KU PO-MO-KO Pale ali poingia / Mule ali motokea /
Kule ali kofunga
ZOEZI
1. Fafanua dhana ya sarufi kisha eleza tanzu
zinazoijenga.
2. Eleza umuhimu wa kujifunza sarufi ya Kiswahili.
3. Onesha tofauti iliyopo kati ya irabu na konsonanti.
4. Eleza maana ya silabi na uoneshe kwa mifano
miundo mitano ya Silabi za Kiswahili.
5. Nini maana ya mofimu? Fafanua aina zake.
6. Bainisha dhima za kila mofimu katika maneno
yafuatayo:
a. Anakula
b. Waliokutafuta
c. Tulipokukosa
d. Nikikukumbuka
e. Aliyempigia
f. Hakufika
g. Huimba
h. Mnavyopendana
i. Amemtukana
j. Ungelifika
7. Nini maana ya uambishaji na mnyumbulkiko wa
maneno? Onesha jinsi dhana hizo zinavyochangia
kukuza lugha.
8. Eleza kauli mbalimbali za vitenzi vya lugha ya
Kiswahili.
9. Pachika viambishi ngeli vya O- rejeshi katika vitenzi
vifuatavyo ukibainisha umoja na uwingi:
a. Chura amekufa
b. Kitabu kimechanika
c. Meza imevunjika
d. Daftari limechanika
e. Simu imeita
f. Ameingia mahali humu
g. Amepitia pale
h. Imevunjiwa kule
10. Neno
Ni silabi au mkusanyiko wa silabi
zinazotamkwa au kuandikwa ambazo huwa na
maana (maana yaweza kuwa ni ya kileksika au
kisarufi).
AINA ZA MANENO
1. NOMINO
Ni aina ya neno ambalo hutaja mtu, kitu,
mahali, hali na kitendo. Mfano; Mwajuma, Kalamu,
Mwanza, Udakitari, Kulima n.k.
Aina za nomino:
Nomino za pekee: Nomino za pekee hutaja
na kutambulisha nomino mahsusi na za kipekee.
Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si chengine
chochote. Hizi ni nomino zinazohusisha majina
kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima,maziwa
na bahari. Herufi za kwanza za nomono za pekee
huwa kubwa hata kamanomino hizi zinapatikana
katikati ya sentensi. Mfano; baba, Asha, Tanzania,
Dodoma, Kilimanjaro, Victoria n.k.
Nomino za jamii: Hizi kwa jina jengine
huitwa nomino za jumla. Nomino hizihazibainishi
wazi wazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa.
Kwa mfano ikiwa nimtu, mahsusi hatambuliwi.
Haituambii kama ni Kelvin, Tuafu ama
Zawadi.Ikiwani ziwa halitambuliwi kama ni
Michigan , Victoria au Nyasa, yaani hutaja vitubila
kutaja umahsusi wake kama ilivyo katika nomino za
pekee. Hizizinapoandikwa si lazima zianze kwa
herufi kubwa isipokuwa zimetumiwamwanzoni mwa
sentensi au zimetumika kama anuani ya kutajia kitu
kama vileMkuu wa Sheria. Katika mfano huu
‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida,lakini
hapa inaanza kwa herufi kubwa kwani inataja
anuwani ya kipekee. Mfano wa nomino za kawaida
ni; Mwanafunzi, Mwalimu, Mnyama, Mtazamaji,
Askari n.k.
Nomino za kawaida: Kundi hili la nomino
hutumia kigezo cha uwezekano wakuhesabika
kuziainisha. Hapa tunatofautisha kati ya nomino
zinazowakilisha vitu vinavyohesabika kwa upande
mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande
mwengine. Nomino ya vitu vinavyohesabika vitanda,
nyumba, vikombe vitabu kadahlika. Zile
zisizohesabika hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa
wingi na haviwezi kugawika, kwa mfano maji, mate,
makamasi, maziwa, moshi, mafuta. Aghlabu nomino
hizo huwa sawa katika umoja na wingi.
Nomino za kitenzi jina: Hizi ni nomino
zinazohusu vitenzi . Huundwa kwa kuongezwa
kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa
kitenzi cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino.
Mfano; Kulima, Kucheza, Kuimba n.k.
Nomino dhahania: Hizi ni nomino ambazo
hurejelea vitu vinavyoweza kuhusika na
mwanaadamu kupitia milango ya hisia kama macho,
mapua, masikio vidole na ulimi- yaani vitu ambavyo
haviwezi kushikika, kuonekana, na kuonjeka. Mfano;
Vita, Njaa, Ugonjwa, Shetani, Mungu n.k.
2. VIVUMISHI
Ni maneno ambayohutoa ufafanuzi au
maelezo ya ziada kuhusu jina ili kuitambulisha
vyema.
Aina za vivumishi:
Vivumishi vya sifa: hutoa sifa za nomino /
kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza kuwa
nzuri, mbaya au yoyote ile.Mfano; mzuri, mbaya,
mrembo n.k.
Vivumishi vya idadi: vinaweza kujitokeza
katika aina tatu ndogondogo.Vivumishivya aina hii
hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo
kiwango chakekimetajwa. Mfano; wawili, watano,
wengi, wachache n.k.
Vivumishi vya kumiliki: Ni vivumishi
vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina milikiwa na
mtu au kitu chengine. Mfano;yangu, yake, yako,
kwetu n.k.
Vivumishi Vioneshi: Vivumishi vya aina hii
huonyesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi
vya aina hiihujengwa na mzizi {h} kwa vitu vilivyopo
karibu na mzizi {le} kwa vitu vilivyo mbali. Mfano;
hapa, pale n.k.
Vivumishi vya kuuliza: Hivi ni vivumishi
ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari
zake. Hujibu swali “gani? ipi? ngapi?”
Vivumishi vya pekee: Vivumishi hivi huitwa
vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na
maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua
upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli
yanomino ambayo kinaivumisha. Mizizi vivumishi
hivi ni -ote, -o-ote, -enye, -enyewe, -ingine, -
ingineo, -ote. Huonyesha ujumla wa kitu au vitu-o-
oteKivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila
kubagua”– enyeKivumishi cha aina hii hutumika
kuleta dhanna ya umilikishaji nomino Fulani. –
enyeweKivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza
nomino fulani.– ingineKivumishi cha aina hii
huonyesha/huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu
Fulani. – ingineoKivumishi cha aina hii hutumika
kuonesha/kuonyesha ziadi.
Vivumishi vya A- unganifu: Vivumishi vya
aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a-
unganifu. Kihusishi hikihuandamana na nomino
kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino
iliyotajwaawali. Vivumishi vya aina hii hutumika
kuleta dhanna zifuatazo: -Umilikaji-Nafasi katika
orodha. Mfano; wa kwangu, wa Juma, ya tano ya
Sita n.k.
3. VIELEZI
Maana ya vielezi: Vielezi ni maneno
yanayofafanua vitenzi, vivumishi auvielezi vyengine.
Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka
wapi , namnagani na hata mara ngapi?
Aina za vielezi
Vielezi vya namna au jinsi. Vielezi vya
namna hii huonyesha jinsi au namna kitendo
kilivyotendeka. Vielezi vyanamna vipo vya aina
kadhaa.
Vielezi vya namna halisi
Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo
kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa moja katika
uainishaji wa aina za maneno. Mfano; kuimba sana.
Vielezi vya namna mfanano
Hivi ni vieleziambavyo hutumika kufananisha
vitendo na vivumishi au nomino mbalimbali.
Hujengwa kwa kuongeza kiambishi (ki-) au
kiambishi (vi-). Viambishi hivi hujulikana kwa jina la
viambishi vya mfanano.Ulifanya vizuri kumsaidia
mwanangu.
Vielezi vya namna vikariri
Hivi nivieleziambavyo hufafanua vitenzi kwa
kurudiarudia neno moja mara mbili.Mfano; polepole,
harakaharaka.
Vielezi vya namna hali
Hivi nivieleziambavyo hufafanua juu ya kitendo
kilichotendeka kimetendeka katika hali gani. Mfano;
kivivu, kibabe, kizembe, kipole n.k.
Vielezi vya namna ala/kitumizi
Hivi nivielezi vinavyotaja vitu ambavyo hutumika
kutendea kitendo. Mfano; kwa kisu, kwa kalamu n.k.
Vielezi vya namna viigizi.
Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa
kuigiza au kufuatisha sauti inayojitokeza wakati
tendo linapofanyika au kutokea. Mfano; alimpiga
paaaah!
Vielezi vya idadi. Vielezi vya namna hii
huonyesha kuwa kitendo kilitendeka mara fulani au
kwa kiasifulani. Mfano; amempiga mara mbili.
Vielezi vya mahali. Vielezi vya namna hii
huonyesha mahali ambapo kitendo
kinatokea.Huweza kudokezwakwa viambishi au kwa
maneno kamili. Mfano; amekaa jikoni.
Vielezi vya wakati:Vielezi vya namna hii
huonyesha wakati wa kutendeka kwa
kitendo.Huweza kutokeakama maneno kamili au
hodokezwa kwa kiambishi {po.}Mfano; alimkaribisha
alipokuja.
4. VITENZI
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo
lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu
lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote
kinachoweza kutenda jambo. Kitenzi cha Kiswahili
huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye
uamilifu wa aina tofauti.
AINA ZA VITENZI
Vitenzi vikuu (T): Vitenzi vikuu ni vile
ambavyo hubeba ujumbemuhimu wa kiarifu cha
sentensi. Mfano; Mtoto amekuja.
Vitenzi visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya
kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile
uwezekano , wakati, hali n.k. Vitenzi visaidizi daima
hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba
viambishi vya wakati. Mfano; Alikua anacheza,
Huwa namfurahia.
Vitenzi visaidizi huweza kupachikwa urejeshi wa
nomino na kusaidia kuifafanua nomino hiyo. Mfano;
motto aliyekua anacheza. Virejeshi hivyo ni kama; -
ye-, -yo-, -o-, -lo-, -cho-, -wo- n.k
Vitenzi vishirikishi: Hivi ni Vitenzi ambavyo
hufanya kazi ya kuunga sehemu mbili za sentensi.
Havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama
hali.Vitenzi vishirikishi ni vya aina mbili, ambavyo
nikitenzi kishirikishi “ni” cha uyakinishi na kitenzi
shirikishi “si” cha ukanushi.
Kazi za kitenzi kishirikishi
- kushirikisha vipashio vingine katika sentensi
- kuonesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya
mtu fulani au kitu fulani
- kuonyesha cheo au kazi anayofanya mtu
- kuonyesha sifa za mtu
- kuonyesha umoja wa vitu au watu
- kuonyesha mahali
- kuonyesha umilikishi wa kitu chochote.
5. KIWAKILISHI
Kiwakilishi ni aina ya neno linaloweza kutumika
badala ya jina . AINA ZA VIWAKILISHI Viwakilishi
vya kuuliza/viwakilishi viulizi ambavyo huashiriwa
na mofu / kiambishi {-pi} ambavyo katika tungo
hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika.
Mfano- Mtoto yupi Wiwakilishi vya urejeshi
ambavyo vinajengwa na shina amba pamoja na
vipande vidogo vidogo –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po,
mo, ko n.k ambavyo vinachaguliwa kilingana na
ngeli ya majina yanayorejeshwa navyo. Viwakilishi
vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya
nomino hiyo huweza kuwa kamili (halisi) au ya
jumla. Mfano; Wengi wamekuja Viwakilishi vya
pekee:-Hivi ni aina ya vivumishi vya pekee
kuwakilisha nomino. Hufuata sheria za upatanisho
za nomino zinazowakilishwa. Viwakilishi vya A-
unganifu:-Viwakilishi hivi huundwa kwa kihisishi
cha A-unganifu kusimamia nominoiliyomilkiwa,
inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino
ya aina fulani.Kihisishi a-unganifu huandamana na
nomino kuunda kirai husishi ambacho
husimamamahali pa nomino.
6. VIUNGANISHI
Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi
chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi au
sentensi.Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio
viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi. Aina za
viunganishi: · Viunganishi huru: hivi ni viunganishi
vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya
vipashio vinavyo ungwa. Hujumuisha: - -Viunganishi
nyongeza/vya kuongeza. Mfano; Tena,Na,Zaidi ya
n.k. - Viunganishi vya sababu/visababishi. Mfano;
Kwa kuwa,kwa sababukwa vile, kutokana na, n.k. -
Viunganishi linganishi/vya kinyume. Mfano; Ingawa,
Japokuwa, Lakini n.k. - Viunganishi vya wakati.
Mfano; kasha, baadaye, Halafu, Baada ya n.k. -
Viunganishi vya masharti. Mfano; Kama, Ikiwa,
Iwapo n.k - Viunganishi vihusishi Mfano; Cha, La,
Wa, Za n.k. · Viunganishi tegemezi: Ni viambishi
ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi
ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru
ambavyo kwa pamoja huunda sentensi
changamano au shurtia. Mfano; -ye-, -po-, -ki-, -
cho- na -nge-.
7. VIHUSISHI
Ni maneno ambayo huonyesha uhusiano uliopo
baina ya neno moja na jengine.Vihusishi aghlabu
huonyesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino
na maneno mengine. Mambo mbalimbali
yanayoweza kuonyeshwa na vihusishi - huonyesha
uhusiano wa kiwakati - huonyesha uhusiano wa
mahali - huonyesha uhusiano wa kulinganisha -
huonyesha uhusiano wa umilikaji - huonyesha
uhusiano wa sababu/kiini Aina za vihusishi -
vihusishi vya wakatiMfano; kabla ya, baada ya n.k -
vihusishi vya mahaliMfano; chini ya, juu ya, ndani
ya, mbele ya n.k. - vihusishi vya ulinganishi/ vya
kulinganisha Mfano; kuliko, zaidi ya n.k. -vihusishi
vya sababu/ kusudi/nia Mfano; kwa sababu ya, kwa
ajili ya n.k. -vihusishi vya ala (kifaa)-Mfano; kwa -
vihusishi vimilikishi Mfano; cha, za n.k. -vihusishi
vya namna/jinsi/hali Mfano; moto wa kuotea mbali,
macho ya mviringo Matumizi ya ziada ya kihusishi
“kwa” -kihusishi hiki huonyesha mahali au upande -
kihusishi hiki huonyesha sababu au kisababishi cha
jambo -kihusishi hiki huonyesha wakati -kihusishi
hiki huonyesha sehemu Fulani ya kitu kikubwa -
kihusishi hiki hutumika kuonyesha ‘nia ya pamoja
na’ -Kihusishi hiki huonyesha jinsi kitendo
kilivyotendeka
Yuri Zimin, 2015
Источник: http://e-kayumba.blogspot.com/(1)
http://e-kayumba.blogspot.com/(2)
http://e-kayumba.blogspot.com/(3)
http://e-kayumba.blogspot.com/(4)
Friday, August 16, 2024
MADENI YA PARKING ( MAEGESHO )
Jinsi ya Kulipa Ushuru wa Maegesho ya Magari | How to Pay Parking Fee in Tanzania
The following below are instructions on how you can check parking fee and make payment;
- Visit https://termis.tarura.go.tz/#/welcome
- Then click Pay ‘Lipa’
Where you will be directed to page of writing your car number and click search button.
You will get results if there is debt and mode of payment.
Alternatively can download TERMIS App to check Jinsi Ya Kuangalia Deni La
Pay parking Fees Using USSD Code
- Bonyeza *152*00#
- Chagua namba 4 (Nishati, madini na usafiri)
- Baada ya hapo chagua namba 2 (Tarura)
- Kisha chagua namba 2 (Termis/angalia deni)
- Ingiza namba ya usajiri wa chombo cha usafiri mf. T544 AZZ
- Utapokea ujumbe mfupi wenye deni lako na kumbukumbu namba ya malipo.
Jinsi ya kulipia car parking
- Bonyeza *152*00#
- Chagua namba 4 (Nishati, madini na usafiri)
- Baada ya hapo chagua namba 2 (Tarura)
- Kisha chagua namba 1(Lipia Maegesho)
Thursday, August 15, 2024
Sunday, August 11, 2024
Monday, August 5, 2024
General Criteria for First-Year Applicants:
- Citizenship: Must be a Tanzanian citizen.
- Age: Must be no older than 35 years old at the time of application.
- Admission: Must have secured full-time admission to an accredited higher education institution in Tanzania, including the Open University of Tanzania (OUT).
- Application: Must have submitted a complete and accurate application through the Online Loan Application and Management System (OLAMS).
- Employment: Must not have a formal or regular income from employment or an established contract in either the public or private sector.
- Previous Loan Repayment: For students who have previously dropped out or discontinued their studies, proof of repayment of at least 25% of any prior HESLB loan is required.
- Completion of ACSEE: Must have completed the
Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSEE) or an
equivalent qualification within the past five years (from 2019 to 2023
inclusive).
kuomba ingia link : https://olas.heslb.go.tz/olams/pre-applicant
Wednesday, July 31, 2024
Friday, July 19, 2024
Kozi zinazolipa kwa haraka na malipo ya juu:
1. Diploma in Mobile Repairing
2. Diploma in Food Technology
3. Diploma in Digital Marketing
4. Diploma in Interior Designing
5. Diploma in Travel and Tourism Management
6. Diploma in Pharmacy
7. Diploma in Event Management
8. Diploma in Graphic Designing
9. Diploma in Fashion Designing
10. Diploma in Computer Hardeware and Networking
Tuesday, June 25, 2024
Sunday, June 23, 2024
Saturday, June 22, 2024
Na Mwandishi Mbojo,
Zifuatazo ni siri za kufaulu endapo utazizingatia:
1. Kusoma kwa bidii
2. Kuwa na vitabu vinavyoenda na wakati
3. Kuwa na mbinu nzuri za kusoma
4. Kuwa ratiba unayoiheshimu ( Nidhamu ya muda )
5. Kujiwekea malengo
6. Kujifanyia taathimini mara kwa mara
7. Kujiamini unaweza
8. Kupata burudani kwa kucheza baada ya masomo ( Mapumziko )
9. Kutafuta ufumbuzi wa changamoto za masomo
10. Kulala mapema na kuamka mapema.